Rasmi: Chelsea yathibitisha uhamisho wa Hakim Ziyech - Darajani 1905

Rasmi: Chelsea yathibitisha uhamisho wa Hakim Ziyech

Share This
Klabu za Chelsea na Ajax Amsterdam zimethibitisha kufanya biashara ya nyota raia wa Morocco, Hakim Ziyech ambaye atajiunga na Chelsea kwenye dirisha kubwa lijalo.


Usajili huu unatajwa kuigharimu Chelsea kiasi cha euro milioni 40, dau ambalo linaweza kupanda na kufikia euro milioni 44 kutokana na baadhi ya vipengele vilivyomo kwenye mikataba hiyo ya makubaliano.

Inaelezwa kwamba nyota huyo mwenye miaka 26 atasaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia Chelsea na atalipwa mshahara unaofikia euro milioni 5 kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment