Chelsea yavuna alama tatu muhimu, yausogelea ubingwa - Darajani 1905

Chelsea yavuna alama tatu muhimu, yausogelea ubingwa

Share This
Chelsea inapata ushindi mwengine wa ligi kuu Uingereza kwa soka la wanawake na kuzidi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.


Usiku wa leo mara baada ya kuhairisha mchezo dhidi ya Man utd Women kutokana na hali mbaya ya hewa Chelsea imeshuka uwanjani usiku wa leo ambapo mchezo umeisha uku Chelsea ikichukua alama zote tatu na kuzidi kuweka rekodi ya kuwa timu pekee ambayo haijafungwa mpaka sasa.


Wafungaji wa mabao ya leo ni Guro Reiten ambaye alifanya mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Chelsea Women inaongoza bao 1-0 kabla ya Bethany England kuja kuongeza bao la ushindi kipindi cha pili na kuwa goli lake la 13 kwenye michuano hii ya ligi kuu.

Matokeo haya yanaifanya Chelsea kutimiza alama 38 uku ikicheza michezo 14 ikiwa na vipolo vya michezo miwili.

No comments:

Post a Comment