Kocha Ajax atoa neno Ziyech kuhusishwa kutua Chelsea - Darajani 1905

Kocha Ajax atoa neno Ziyech kuhusishwa kutua Chelsea

Share This

Vyanzo vingi vya habari vimekuwa vikiripoti taarifa ya Chelsea kutajwa kufikia makubaliano ya kumnasa nyota wa Ajax, Hakim Ziyech.

Kocha wa klabu hiyo, Erik ten Hag amefanyiwa mahojiano na kuulizwa kuhusu taarifa hizo zinazomtaja winga huyo nyota raia wa Morocco kuhusishwa kutakiwa na Chelsea.


"Ziyech kwenda Chelsea? mbina ni usajili tuliokuwa tunautegemea kutimia miaka miwili au mmoja uliopita, ilikuwa kila dirisha likifungwa tunasema heeh hatimaye bado tupo nae. Tunafuraha maana ataendelea kuwa nasi mpaka msimu utakapoisha." amesema kocha huyo.

Kwa mujibu wa taarifa inaelezwa kwamba nyota huyo amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia Chelsea kuanzia msimu ujao uku mshahara wake ukitajwa kufikia euro milioni 5 kwa mwaka pamoja na bonasi.

Nyota huyo mwenye miaka 26 ni raia wa Morocco ingawa alizaliwa nchini Uholanzi ambapo ndipo alipotumia muda wote wa maisha yake ya soka kucheza nchini humo.

No comments:

Post a Comment