Chelsea dimbani usiku wa leo kupambania taji la ligi kuu - Darajani 1905

Chelsea dimbani usiku wa leo kupambania taji la ligi kuu

Share This

Bethany England akipiga picha na baadhi ya mashabiki wa Chelsea Women
Usiku wa leo majira ya saa nne Chelsea Women itarejea uwanjani mara baada ya mchezo uliopita kuhairishwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Leo Chelsea Women itakuwa nyumbani Kingsmeadow kucheza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza kwa soka la wanawake maarufu kama Barclays FA WSL ambapo wataikaribisha klabu ya wanawake ya Birmingham.

Kiungo Ji So-Yun akiwasili uwanjani

Mchezo huo ni nafasi kwa Chelsea kuzidi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo ambapo wanakimbizana kwa karibu na Man city Women na Arsenal Women.

No comments:

Post a Comment