Nyota wa Chelsea awania tuzo ya mchezaji bora - Darajani 1905

Nyota wa Chelsea awania tuzo ya mchezaji bora

Share This

Nyota wa Chelsea Women ambaye ni nyota mpya klabuni hapo, Samantha Kerr amechaguliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa soka la wanawake.


Nyota huyo raia wa Australia ambaye ata sasa yupo na timu yake ya taifa uku Chelsea Women ikishuka uwanjani usiku wa leo kucheza mchezo wake wa ligi kuu amechaguliwa kuwania tuzo hiyo inayotolewa na shirika la habari nchini Uingereza maarufu kama BBC ambapo huwa na kawaida ya kutoa tuzo kwa wanasoka na wanamichezo wa michezo tofauti tofauti waliokuwa bora kwa mwaka mzima.

Washiriki wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na:
Lucy Bronze
Julie Ertz
Samantha Kerr
Vivianne Miedema
Megan Rapinoe

No comments:

Post a Comment