Chelsea yakamilisha makubaliano ya kumnasa Ziyech wa Ajax - Darajani 1905

Chelsea yakamilisha makubaliano ya kumnasa Ziyech wa Ajax

Share This
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa na vinavyoaminika inaelezwa kwamba klabu ya Chelsea imefikia makubaliano na klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi juu ya usajili wa nyota, Hakim Ziyech.


Inaelezwa kwamba klabu hizo zimefikia makubaliano ya nyota huyo anayecheza nafasi ya winga wa kulia kuigharimu Chelsea dau la euro milioni 45.

Nyota huyo raia wa Morocco ingawa alizaliwa nchini Uholanzi ana umri wa miaka 26 na soka lake kuanzia ngazi ya mtoto mpaka sasa amelicheza nchini Uholanzi akisajiliwa na Ajax mwaka 2016 akitokea klabu ya FC Twente.

No comments:

Post a Comment