Chelsea yakaa kikao na Sassuolo kukamilisha uhamisho wa Boga - Darajani 1905

Chelsea yakaa kikao na Sassuolo kukamilisha uhamisho wa Boga

Share This
Taarifa zinazoripotiwa na magazeti kadhaa ya barani Ulaya ni kwamba mkurugenzi wa michezo na mwenyekiti wa bodi ya Chelsea, Marina Granovskaia leo atakutana na uongozi wa klabu ya Sassuolo ili kukamilisha biashara ya nyota kinda wa klabu hiyo, Jeremie Boga.

Chelsea inataka kumsajili tena nyota huyo kinda ambapo dau la paundi milioni 12 linatajwa kutumia kumsajili nyota huyo aliyekuwa mchezaji wa Chelsea kabla ya kujiunga na Sassuolo mwaka 2018 akiondoka Chelsea aliyoichezea mchezo mmoja.

Boga mwenyewe aliwai kuhojiwa na akasema yupo tayari kurejea Chelsea kama usajili huo ukikamilishwa.

No comments:

Post a Comment