Real Madrid yazidi kumfikiria Thibaut Courtois - Darajani 1905

Real Madrid yazidi kumfikiria Thibaut Courtois

Share This

Klabu ya Real Madrid inatajwa bado kuwa kwenye mpango wa kumsajili mlinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtois kama mbadala endapo itashindwa kumnasa mlinda mlango wa Man utd, David de Gea.

Taarifa zilizopo zinadai kuwa klabu hiyo ya nchini Hispania inamtaka de Gea kama chaguo lake la kwanza katika dirisha kubwa la usajili lijalo ingawa kama itashindwa kumnasa mhispania huyo basi itajitosa kwa Courtois ili kumsajili.

Nyota huyo raia wa Ubelgiji aliwai kuichezea kwa mkopo klabu ya Atletico Madrid inayopatikana jiji moja na klabu ya Real Madrid na alishawai kukiri kuwa bado moyo wake upo jijini Madrid, kauli iliyotafsiriwa na wachambuzi wengi kuwa hataki kuendelea kusalia klabuni Chelsea na alisema kauli hiyo ili kuifanya klabu hiyo ifanye haraka ili imsajili ingawa mwenyewe alikanusha kwa kusema kauli yake hiyo ni kutokana na familia yake ya mke na watoto wawili kuendelea kuishi jijini huko.

No comments:

Post a Comment