KITAMBO; KUELEKEA MCHEZO WA CHELSEA vs Barca, UNAIKUMBUKA HII? - Darajani 1905

KITAMBO; KUELEKEA MCHEZO WA CHELSEA vs Barca, UNAIKUMBUKA HII?

Share This
Kesho Chelsea itakuwa uwanjani kumenyana dhidi yaa Barclona katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya ambapo mchezo huo utachezwa nchini Hispania kwa mchezo wa marudiano. Karibu mashabiki wote duniani ukiwauliza juu ya mchezo huu na nini wanakikumbuka zaidi basi kuna matukio ambayo atakutajia ambayo anayakumbuka vyema.

Atakutajia matukio mengi ambayo sanasana yatakuwa yale magoli ya Ronaldinho akiifunga Chelsea mwaka 2004 ambapo Chelsea ilishinda mchezo huo kwa magoli 4-2, atakutajia lile goli la Fernando Torres katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 2012 pale Camp Nou, goli ambalo liliwanyong;onyesha wachezaji wa Barcelona lakini pia atakutajia ule ukatili uliofanywa na mwamuzi wa mchezo wa hatua ya nusu fainali ya mwaka 2009 ambapo Chelsea ilikataliwa penati zake za wazi kabisa katika mchezo dhidi ya Barcelona uliohezwa Stamford Bridge, nami nipo hapa nataka nikukumbushe kuhusumchezo huo na nini kilimtokea kocha huyo mara baada ya mchezo huo kuisha.

Anaitwa Tom Henning Ovrebo, moja kati ya waamuzi walioingia kwenye orodha ya kuchukiwa na mashabiki wa Chelsea duniani kote. Ukiwaulizwa  mashabiki wa Chelsea kote duniani kwamba ni mwamuzi gani wanamchukia basi nadhani jina la huyo raia wa Norway ndilo litakalotajwa zaidi.

Ilimchukua dakika 90 tu kuchukiwa zaidi na mashabiki wa Chelsea lakini pia na mashabiki wa soka duniani kote. Alikuwa mwamuzi kwenye mchezo wa Chelsea dhidi ya Barcelona kama utakavyokuwa mchezo wa kesho, ingawa huu wa kesho tofauti yake na huu naokukumbusha ni kwenye kiwanja kilichotumika, huu mchezo wa kesho utachezewa Camp Nou nchini Hispania wakati huu naokukumbusha ulichezwa Stamford Bridge na tofauti nyengine ni hatua ya mchezo, ambapo huu wa kesho utakuwa hatua ya 16 bora wakati huu naokukumbusha ulikuwa hatua ya nusu fainali.

Turudi kule sasa, mchezo wa kwanza uliochezwa Camp Nou uliisha kwa sare ya 0-0 na sasa mchezo ulikuwa upo Stamford Bridge huku kocha wa Chelsea kipindi iko akiwa Gus Hiddink. Alipanga kikosi chake kikiwa kamili, Didier Drogba, Michael Essien, Frank Lampard, Michael ballack, john Terry yani kilikuwa kamili gado huku kwa Barcelona nyota wao akiwa ni Lionel Messi pamoja na Eto'o.

Mechi ilikuwa kali na yenye mvuto mkubwa lakini raha na utamu wa mchezo huo iliharibiwa na mwamuzi huyo ambaye alionekana dhahiri aliwabeba Barcelona. Mpaka leo mwandishi nashangazwa na tukio alilolifanya Ballack la kumfokea mwamuzi huyo mara baada ya kushangazwa na maamuzi yake lakini kinachonishangaza kwanini mwamuzi huyo hakumuonyesha kdi nyekundu, ndio hapo napoamini kuwa mwamuzi alijua alifika uwanjani kwa kazi moja tu ya kuibeba klabu hiyo maana kama angekuwa yupo sawa alikuwa na haki zote za kumuonyeshea kadi nyekundu mjerumani huyo.

Mara baada ya mchezo huo kupita, ilipita miaka mitatu, na kocha huyo alikiri kuna mashabiki wa Chelsea mpaka leo hii wanamtumia ujumbe wa kumtishia maisha, halikuwa jambo zuri kumtumia jumbe hizo, lakini kama ukiangalia matukio aliyoyafanya mwamuzi huyo inatia hasira.

Mwaka huu, 2018 alifanyiwa mahojiano na chombo kimoja juu ya mchezo huo na mwamuzi huyo alikiri kwamba hakuwa sawa kimaamuzi. Aliiangusha Chelsea. Lakini maneno yake hayasaidii kitu, na hayafanyi mashabiki wa Chelsea wamuone kama ni mtu mwema maana aliikandamiza bila huruma.

No comments:

Post a Comment