Nyota wa Chelsea, Ruben Loftus-Cheek aliyekuwa akiichezea kwa mkopo klabu ya Crystal palace kabla ya kupata majeraha ameungana tena na klabu hiyo ya Crystal palace ambayo ameungana nayo ili kumalizia mkataba wake wa mkopo.
Nyota huyo alipata majeraha yaliyomfanya akae nje kwa muda mrefu sasa anatajwa kuruhusiwa kujiunga na klabu ya Crystal Palace ili amalizie mkopo wake mara baada ya kupata majeraha na kurudi klabuni Chelsea ili kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Taarifa zinadai kwamba nyota huyo alifanya mazoezi na kikosi cha Chelsea cha chini ya miaka 23 wiki iliyopita na sasa anaonekana kuimarika na kuwa sawa hivyo kuonyeshwa taa ya kijani kuungana tena na klabu hiyo ambayo nayo inapatikana kwenye jiji la London
LOFTUS-CHEEK NJIANI KURUDI CRYSTAL
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment