Chelsea kesho itakuwa uwanjani kucheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Barcelona katika hatua ya raundi ya 16 bora katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya ambapo mchezo huo utachezwa nchini Hispania kwenye uwanja wa Camp Nou
Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha Antonio Conte amewapa tahadhari wachezaji wake kuelekea kwenye mchezo huo ambapo atakayeshinda au kufanikiwa kufudhu kwenye hatua hiyo basi atacheza hatua inayofata ambayo ni hatua ya robo fainali.
"Ni muhimu kuelewa inatakiwa tujiandae kupambana, kama tutacheza na Hazard kama namba 9 (mshambuliaji wa kati) au hata kama tukicheza na Morata au Giroud akama namba 9 na Hazard kama namba 10"
"Inatakiwa tucheze kama tulivyocheza kwenye mchezo uliopita pale Stamford na inatakiwa tukipata nafasi tuhakikishe tunazitumia kufunga magoli" alisema kocha huyo.
Chelsea itahitaji matokeo sare ya kuanzia 2-2 au kuendelea au ipate ushindi ili ifanikiwe kupata nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali wakati kwa upande wa Barcelona ili afanikiwe kufudhu anahitaji aifunge Chelsea au apate sare ya 0-0.
HAZARD, GIROUD AU MORATA NANI KUTUMIKA KESHO? CONTE ATOA TAHADHARI
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment