Kilichopo kwa sasa ni kusubiriwa kwa mchezo wa hapo kesho, mchezo kati ya Barcelona dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Camp Nou, mchezo ambao utaenda kuweka historia mpya kutokana na kuwa na msisimko mkubwa haswa pale zinapokutana.
Katika kujiandaa ili kucheza mchezo huowa hatua ya 16 bora, gwiji wa soka wa Chelsea ambaye ni raia wa Uingereza, Frank Lampard ametoa neno na kumshauri kocha Antonio Conte ni kikosi cha aina gani anapaswa kukipanga ili aweze kuikabili klabu hiyo ya nchini Hispania.
"Napendekeza atumike Morata katika safu ya ushambuliaji, atumike kama mtu wa kati huku akiongozwa na Hazard pamoja na Willian. Morata anatakiwa acheze kwenye ubora tofauti na alivyocheza michezo kadhaa iliyopita. Anatakiwa awe na nguvu na awe ngangari na ajitahidi amiliki sana mpira. Ana uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yake, naamini hilo analiweza"
"Lakini pia jambo jengine ambalo Morata ataipa faida Chelsea kama akitumika ni kutokana na kiasili kuwa mshambuliaji wa kati, sio kama Hazard akitumika katika eneo hilo. Alichokionyesha Torres kwenye mchezo wa 2012 ndicho anachoweza kukifanya mshambuliaji wa kati ambaye kiasili ndiyo nafasi yake" alisema gwiji huyo ambaye kwa sasa anasomea ukocha na anakaribia kumaliza mafunzo ya ukocha kwa daraja A.
LAMPARD AMSHAURI CONTE, AMWAMBIA PIA JUU YA HAZARD NA MORATA
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment