WILLIAN AGOMBANIWA SOKONI - Darajani 1905

WILLIAN AGOMBANIWA SOKONI

Share This
Nyota wa Chelsea, Willian Borges da Silva ambaye kwa sasa ana miaka 29 amekuwa kwenye ubora wa hali ya juu haswa kwenye hii michezo ya mwisho ambapo Chelsea imeshuka uwanjani, ambapo katika michezo mitatu iliyopita, nyota huyo amefunga magoli manne na kufanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania uchezaji bora wa wiki kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya na hata kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombania goli bora la wiki kwenye michuano hiyo.

Kutokana na ubora wake vilabu kadhaa vimekuwa vikitajwa kuanza kumfukuzia nyota huyo raia wa Brazil ambapo sasa klabu ya Ac Milan nayo imetajwa kuanza mipango ya kumuwania nyota huyo ambaye amefanikiwa kushinda mataji kadhaa klabuni Chelsea. Klabu nyengine zinazotajwa kumfukuzia ni pamoja na Real Madri, Barcelona na Manyumbu (Man utd) iliyochini ya kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho.

No comments:

Post a Comment