STERLING, NYOTA ASIYETAJWA SANA KLABUNI CHELSEA - Darajani 1905

STERLING, NYOTA ASIYETAJWA SANA KLABUNI CHELSEA

Share This
Moja kati ya vipaji adimu kwenye akademi ya Chelsea ni huyu nyota kinda anayeichezea Chelsea ya vijana chini ya miaka 18, Chelsea U18 anayeitwa Dujon Sterling. Amekuwa haimbwi sana akicheza chini ya kivuli cha Callum Hudson-Odoi ambaye ndiye anaonekana kuwa nyota zaidi wa kikosi hicho, lakini Darajani 1905 kinda huyu raia wa Uingereza anaweza kuwa nyota mkubwa hapo baadae.

Dujon Sterling jana aliiongoza vyema Chelsea U18s kupata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Fulham U18s iliyokuwa nyumbani, ambapo Sterling aliingia kama mchezaji wa akiba na kufanikiwa kufunga goli la mwisho na kukamilisha ushindi wa mabao hayo yaliyoifanya klabu hiyo kufanikiwa kufudhu kucheza nusu fainali mara tisa katika miaka tisa ya kombe la FA.

Hapa nakuletea video ya nyota huyo alipofunga goli lake hilo.

No comments:

Post a Comment