Kuelekea Kombe la Dunia, Chelsea kuvuna mipesa kibao kutoka FIFA - Darajani 1905

Kuelekea Kombe la Dunia, Chelsea kuvuna mipesa kibao kutoka FIFA

Share This

Chelsea inawachezaji 14 watakaocheza michuano ya kombe la dunia mwaka huu. Ina wachezaji watatu kwenye timu ya Ubelgiji ambao ni Eden Hazard, Michy Batshuayi pamoja na mlinda mlango Thibaut Courtois wakati kwa timu ya taifa ya Nigeria ina wachezaji wawili ambao ni Victor Moses na Kenneth Omeruo. Kwa timu ya taifa ya Uingereza napo inawachezaji wawili ambao ni nahodha mkuu wa Chelsea, Gary Cahill pamoja na kiungo Ruben Loftus-Cheek.

Kwa timu ya taifa ya Ufaransa napo kuna wachezaji wawili ambao ni N'Golo Kante pamoja na Olivier Giroud. Kwa timu ya taifa ya Hispania yupo Cesar Azpilicueta, Denmark yupo Andreas Christensen, Brazil yupo Willian, Ujerumani yupo Antonio Rudiger na Argentina yupo Willy Caballero. Wanatimia wachezaji 14.

Je katika idadi hiyo yote, klabu yao inafaidika na nini kwa wao kuwa nje na kutojiandaa na msimu mpya? ndipo chama cha soka cha dunia (FIFA) ambao wao ndio wasimamizi na waandaaji wa Kombe la Dunia wakaona itakuwa vyema kuanzisha kodi ya kuzilipa klabu zinazotoa nyota wake ili kushiriki michuano hiyo na sasa hiyo imekuwa rasmi na Chelsea itafaidika kwa nyota wake kushiriki michuano hiyo.

Dau la dola za Marekani 8,350 ($8,350) kwa kila mchezaji limetangazwa kutolewa ambapo klabu zinazotoa wachezaji hao zitalipwa kama ada ya siku moja kwa kipindi chote cha michuano hiyo iwe kama mchezaji kacheza au kaishia kukaa benchi.

Kutokana na dau hilo, klabu ya Chelsea itakuwa ni klabu ya tatu duniani kuvuna donge au dau kubwa huku ikiachwa na klabu za Real Madrid na Manchester city.

Real Madrid ya Hispania itavuna paundi milioni 2.9 wakati Man city inayoshika nafasi ya pili itavuna paundi milioni 2.8 na Chelsea itavuna paundi milioni 2.6

No comments:

Post a Comment