Chelsea imekuwa ikihusishwa kumyaka kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Luis Enrique ili kumrithi kocha Antonio Conte klabuni Chelsea, lakini usajili huo unatajwa kusimamishwa kwa sasa ambapo kocha huyo amesema atatua Chelsea mpaka mwisho wa msimu na sio kuchukua mikoba ya Conte katikati ya msimu kama ilivyokuwa ikitajwa mara baada ya Chelsea kupoteza mchezo wake wa pili mfululizo dhidi ya Watford jumatatu.
Lakini kukataa kutua kwa kocha huyo klabuni Chelsea kunatajwa baada ya kuwepo taarifa kuwa amekubali mkataba wa miaka miwili na nusu ili ainoe Chelsea ifikapo mwisho wa msimu huu kama kocha Antonio Conte akiondoka. Sasa swali lililokuwa linahojiwa, je ni nani atakubali kuinoa klabu endapo mkocha Antonio Conte akiondoka katikati ya msimu maana Enrique ashagoma.
Mchana wa leo kuna chombo kimoja cha habari kimetoa taarifa kuwa moja ya viongozi wa klabu ya Chelsea ambaye anahusika na usajili klabuni happo, Marina Glanovskaia anatajwa kumpendekeza aliyekuwa kocha wa klabu ya Watford, Marcos Silva ambaye ni kocha raia wa Ureno ili atue klabuni Chelsea na aiongoze mpaka mwishoni mwa msimu kabla ya Luis Enrique hajatua.
Kocha huyo ambaye aliwai pia kuifundisha klabu ya Hull city anatajwa kutua Chelsea ili kuiongoza kuelekea mwishoni mwa msimu huu haswa katika kipindi hiki ambacho hana timu anayoiongoza mara baada ya kuachana na klabu ya Watford aliyoiongoza vyema kabla ya baadae kuporomoka ubora wake.
Marco Silva anatajwa kuwa kocha anayekaribia kutua Chelsea huku aliyekuwa akitumika mara kadhaa, Gus Hiddink akionekana hakuna matarajio ya kuiongoza tena klabu hiyo licha ya kutumika mara mbili katika kuiongoza Chelsea haswa katika kipindi kama hiki ambacho makocha wamekuwa wakiondoka Chelsea katikati ya msimu.
MARINA AMLETA MRITHI WA CONTE KLABUNI CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment