KOCHA WA BARCA AIPIGA DONGO CHELSEA - Darajani 1905

KOCHA WA BARCA AIPIGA DONGO CHELSEA

Share This
Mpaka sasa inaonekana kimuhemuhe cha mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Chelsea dhidi ya Barcelona katika klabu bingwa ni kama ndio mchezo unaosubiriwa kwa hamu licha ya kusalia siku mbili kufikia siku ya mchezo huo utakaochezwa pale London ambapo Chelsea itakuwa nyumbani.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha wa Barcelona ambaye ameiongoza klabu hiyo kupata ushindi wa mabao 0-2 ikiwa ugenini ikimenyana dhidi ya Eibar.
Kocha wa wababe hao wa Hispania, Ernesto Valverde aliulizwa juu ya jinsi gani anauona mchezo wa timu yake dhidi ya Chelsea na kocha huyo kusema hajali kuhusu Chelsea.
"Tumetoka kutoa suluhu katika michezo miwili mfululizo, kwa hiyo kupata ushindi katika mchezo huu wa leo ni jambo zuri kwetu. Eibar walijaribu kutumia nguvu kubwa kutuzuia lakini mwisho tumepata ushindi muhimu."

"Kuhusu Chelsea, sijali kuhusu wao, kikubwa nachokiangalia kwenye timu ni timu kupata matokeo mazuri" alisema kocha huyo.

Chelsea itacheza dhidi ya Barcelona kwa mara ya kwanza toka zilipokutana mwaka 2012 ambapo ndio ilipokuwa mara ya mwisho kwa Chelsea kucheza na wababe hao, ambapo Chelsea ilifudhu kwa magoli ya jumla mara baada ya mchezo wa kwanza kucheza uliochezwa Stamford Bridge, Chelsea ikishinda 1-0 huku iliposafiri mpaka nchini Hispania ambako huko mchezo huo uliokuwa wa nusu fainali, klabu hizo zilitoka suluhu ya magoli 2-2 na kuifanya Chelsea kufudhu kwa magoli ya jumla ya 2-3.

No comments:

Post a Comment