Neymar aichokoza Chelsea - Darajani 1905

Neymar aichokoza Chelsea

Share This

Nyota wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, Neymar Jr ambaye ni raia wa Brazil ametoa masharti kwa klabu ya Real Madrid ambayo inatajwa kuwania saini yake ili atue kwenye klabu hiyo pinzani na klabu yake ya zamani ya Barcelona ambayo aliichezea kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya PSG kwa uhamisho uliomfanya kuwa mchezaji ghali zaidi duniani.

Sasa najua unajiuliza, Chelsea inaingia vipi kwenye biashara hii lakini inadaiwa na chombo cha habari cha Diario Gol cha nchini Hispania ambalo limeripoti kuwa nyota huyo ameiambia klabu hiyo kuwa kama inahitaji ajiunge nayo basi ni lazima iwasajili wachezaji watatu ambao mmojawao ni Eden Hazard kutoka Chelsea.

Neymar anatajwa kumtaka winga huyo raia wa Ubelgiji ili ajiunge nae pindi atakaposaini kujiunga na Real Madrid. Hii ni taarifa mbaya kwa Chelsea maana hata kocha wa klabu hiyo ya Real Madrid, Zinedine Zidane amekuwa akipendekeza klabu yake imsajili Hazard na kutokana na maneno hayo ya Neymar huenda ikawafanya Madrid waongeze jitihada ili kumnasa kutoka Chelsea.

No comments:

Post a Comment