Chelsea kucheza fainali kombe la FA - Darajani 1905

Chelsea kucheza fainali kombe la FA

Share This

Mchana wa leo klabu ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 ya Chelsea, Chelsea U18s itakuwa uwanjani kucheza mchezo wa kwanza wa fainali ya kombe la FA kwa vijana ambapo itacheza dhidi ya kikosi cha vijana cha Arsenal U18s.

Kikosi cha Chelsea kilichochini ya kocha Jody Morris kitashuka kwenye mchezo huo kupambania nafasi ya kushinda taji hilo kwa mara ya tano katika miaka mitano ya kombe hilo lililochini ya chama cha soka cha nchini Uingereza maarufu kama FA.

"Ni jambo kubwa na muhimu, lakini naamini hilo litakamilika mpaka tukiwavuka Arsenal" alisema kocha huyo alipoulizwa juu ya anafikiria nini wakati Chelsea U18s itakapopambana kuweka rekodi hiyo.

Muda wa mchezo kwa saa za Afrika mashariki ni saa 09:45 usiku (Saa 21:45)

No comments:

Post a Comment