Tarehe kama ya leo miaka 33 iliyopita alizaliwa mwanadada ambaye kwa sasa anaendeleza kuweka historia na kufanya makubwa kwenye soka la wanawake akiichezea klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea, Chelsea Ladies ambapo jina lake kamili anaitwa Anita Amma Ankyewah Asante au anajulikana haswa ukimuita Anita Asante.
Tarehe 27-April-1985 ndio alizaliwa uko nchini Uingereza lakini akiwa na asili ya Afrika kutoka nchini Ghana. Alianza maisha ya soka kwenye klabu ya Arsenal na kuhamia Chelsea ingawa baadae akatoka na kujiunga na klabu nyengine mpaka leo kurejea Chelsea na akitengeneza safu imara ya ulinzi na mara kadhaa akivaa kitambaa cha unahodha kwenye kikosi hicho kilichochini ya kocha Emma Hayes
Nyota huyo anayeichezea timu ya taifa ya Uingereza leo anatimiza miaka 33 na sisi kama mashabiki wa Chelsea tunatumia fursa hii kumtakia heri ya kuzaliwa.
No comments:
Post a Comment