Bachmann asaini mkataba mpya - Darajani 1905

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea, Chelsea Ladies imetangaza kufanikiwa kumsainisha nyota wake raia wa Switzerland, Ramona Bachmann ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo aliyojiunga nayo akitokea Wolfburg.

Ramona Bachmann ambaye kwa sasa ana miaka 27 alipofanikiwa kusaini mkataba mpya alisema "Mara zote nimekuwa natamani kushinda mataji, na ndio maana nimesaini kuwa hapa kwa miaka mitatu maana hapa ni sehemu sahihi kwa kushinda mataji"

Nyota huyo alibakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake klabuni hapo ambapo ukiongeza na miaka miwili aliyosaini mkataba wa leo ndio sawa na miaka mitatu.

Hongera kwake Ramona Bachmann

No comments:

Post a Comment