Moja kati ya majina yaliyopo kwenye orodha ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi ya kocha Antonio Conte klabuni Chelsea ni jina la kocha raia wa Italia anayeifundisha klabu ya Napoli, Maurizio Sarri ambaye anaifukuzia kwa karibu klabu ya Juventus kwenye kugombania taji la ligi kuu Italia.
Klabu hiyo ya Napoli imekuwa ikikataa kumruhusu kocha huyo kuondoka klabuni hapo ambapo rais wa klabu hiyo, Aurelio De Laurentiis amekuwa akijaribu kufanya mazungumzo na kocha huyo ili asaini mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu ila taarifa zinadai jitihada za rais huyo zimegonga mwamba.
Moja ya magazeti ya nchini Italia limeripoti kuwa klabu hiyo inajiandaa kuwa na maisha mapya ikiwa bila ya kocha huyo Sarri mara baada ya klabu hiyo kuorodhesha majina matatu ya makocha inayowafukuzia ili kurithi nafasi ya Sarri klabuni hapo.
Makocha hao wanaotajwa ni pamoja na kocha wa Sampdoria, Marco Giampaolo, kocha wa Shakhtar Donetsk, Paulo Fonseca na kocha wa Schalke 04, Domenico Tedesco wote wanatajwa kutakiwa na klabu hiyo ambapo hii inatafsiriwa kufungua milango kwa klabu ya Chelsea ipeleke na ianze maombi kwa kocha Maueizio Sarri ili arithi nafasi ya muitaliano mwenzake klabuni Chelsea, Antonio Conte
No comments:
Post a Comment