Nadhani umeipata ile habari inayomhusu kocha wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Manchester united, Jose Mourinho juu ya kauli aliyoitoa kuhusu kutupiwa lawama na watu wengi kwa kushindwa kumpatia nafasi winga raia wa Misri, Mohammed Salah ambaye hakuwa na maisha marefu klabuni Chelsea toka aliposajiliwa mwaka 2014 na kuishia kuichezea michezo 19 na kuifungia magoli mawili huku kwa sasa anaichezea klabu ya Liverpool ambayo mpaka sasa ameshaichezea michezo 47 na kuifungia magoli 43. Kama haujafanikiwa kusoma alichokisema, bonyeza hapa
Mara baada ya maneno hayo ya kocha huyo raia wa Ureno kocha wa Chelsea ambaye ni raia wa Italia, Antonio Conte naye ametoa neno kuhusu maneno hayo ya kocha huyo.
"Hili sio jambo jepesi kwa sababu nadhani inatakiwa tumfananishe Salah wa leo na Salah wa miaka minne au mitano iliyopita. Salah huyu wa sasa ameimalika sana. Ameimarika na kuwa sawa, kucheza kwake Italia kulimsaidia sana kupata uzoefu na kukuza kipaji chake"
"Kwa sasa naamini amekuwa mchezaji wa tofauti na mwenye hali kubwa kimchezo na hata kiubora ukilinganisha na alivyokua mwanzo" alisema Antonio Conte.
No comments:
Post a Comment