Salah azidi kuibua makubwa Chelsea, Mourinho avunja ukimya - Darajani 1905

Salah azidi kuibua makubwa Chelsea, Mourinho avunja ukimya

Share This

Kocha wa Manchester united, Jose Mourinho aliyewai kuifundisha Chelsea amekuwa akipokea lawama na maswali mengi huku akilaumiwa na kuhusishwa kutokufanya vizuri kwa winga raia wa Misri, Mohammed Salah pindi alipokua akiichezea Chelsea kabla ya sasa kuwa moja ya wachezaji tishio akiwa kwenye klabu ya Liverpool.

Kuondoka kwa nyota huyo huku akiichezea Chelsea michezo 19 tu kumekuwa kukimfanya kocha huyo kulaumiwa na wengi kwa kushindwa kukikuza kipaji na uwezo wa nyota huyo ambaye alipotoka Chelsea alijiunga kwa mkopo na klabu ya Fiorentina na baadae alipojiunga na As Roma ambapo huko ndipo alipouzwa kabisa kabla ya Liverpool kumsajili akitokea As Roma katika dirisha kubwa la usajili la mwaka 2017.

Kocha huyo ameamua kuvunja ukimya na kuongea kwa mara ya kwanza sababu haswa iliyomfanya nyota huyo kuondoka Chelsea.

"Mimi ndiye niliyeshawishi asajiliwe Chelsea. Lakini baada ya kusajiliwa nikagundua kuwa kumbe hakuwa bado amekomaa kiakili na hata kihali ya kuwa mchezaji kamili. Nami nikapendekeza atolewe kwa mkopo, naye alikubaliana na mawazo yangu akisema alihitaji muda zaidi wa kucheza"

"Alipotolewa kwa mkopo baadae Chelsea ikaamua kumuuza, lakini mimi sikushawishi auzwe, nilitaka atolewe kwa mkopo. Lakini ninagundua kitu kuwa mpira ni mchezo wa makosa, na makosa yanafanyika. Na kwa kikosi kilichokuwepo sikuamini kama angeweza kuwa bora, kumbuka Chelsea ilikuwa na mawinga kama Hazard na Willian, na mpaka sasa bado wapo" alisema kocha huyo.

No comments:

Post a Comment