Kocha mwengine atajwa kumrithi Conte, mwenyewe atoa maelezo - Darajani 1905

Kocha mwengine atajwa kumrithi Conte, mwenyewe atoa maelezo

Share This

Mpaka sasa kuna fungu kubwa la makocha wanaotajwa kuwania nafasi ya kocha Antonio Conte kwenye klabu ya Chelsea. Makocha kama Luis Enrique, Mauricio Pochettino, Joao Jardim na wengine wengi wanatajwa kuwaniwa na Chelsea ili kurithi mikoba ya kocha huyo raia wa Italia.

Lakini sasa kuna jina jipya limeingia kwenye orodha ya makocha wanaotazamwa na Chelsea ili kuiongoza klabu hiyo kama ikiachana na kocha Antonio Conte.

Ni David Wagner, kocha wa klabu ya Huddersfield ambaye ameiongoza vyema klabu hiyo mpaka kufikia kutunukiwa tunzo ya kocha bora wa mwezi katika ligi kuu Uingereza. Kocha huyo anayetajwa kutakiwa na Chelsea amejibu tetesi hizo za kuhusishwa kutakiwa kwake na Chelsea.

Kocha huyo ambaye kwa sasa anatakiwa pia na klabu za Einthrat Frankfurt na Borrusia Dortmund zote za nchini Ujerumani ambazo alishawai kuzitumikia kama kocha wa kikosi cha akiba, alipohojiwa alisema kwa sasa hafikirii kuachana na klabu hiyo ya Huddersfield na ana mawazo ya kuendelea kuifundisha klabu hiyo msimu ujao licha ya kutakiwa na klabu kubwa kama Chelsea.

No comments:

Post a Comment