Kiungo wa Chelsea, Willian Borges ambaye ni raia wa Brazil huenda akaondoka klabuni hapo ambapo kuna taarifa zinasema kocha Antonio Conte yupo tayari kuachana na nyota huyo ili amvute nyota mwengine raia wa Brazil.
Wilian Borges anaonekana kutokuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza cha Chelsea huku mara kadhaa ikielezwa nyota huyo hana furaha tena a kuendelea kubaki, lakini pia kukielezwa huenda michuano ya kombe la dunia mwakani huko nchini Urusi kunaweza kukamfanya Willian atafute klabu itakayomfanya acheze kila muda ili apate nafasi ya kusafiri na kikosi cha timu ya taifa kuelekea nchini Urusi.
Lakini kuuzwa kwa nyota huyo kunaweza kukafanyika ama kusifanyike ikitegemea kama Chelsea itafanikiwa kumsajili winga mwengine raia wa Brazil anayeichezea klabu ya PSG, Lucas Moura ambaye naye haonekani kutamani kuendelea kubaki klabuni hapo ambapo anakosa nafasi ya kucheza. Thamani ya Moura inatajwa kwa ni paundi milioni 27 ambalo inaonekana Chelsea ipo tayari kukitoa.

WILLIAN KUONDOKA CHELSEA, KUPISHANA NA LUCAS
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment