ASANTENI SANA MASHABIKI WA CHELSEA - Darajani 1905

ASANTENI SANA MASHABIKI WA CHELSEA

Share This
Naanza kwa kumshukuru Mungu mpaka kufikia siku ya leo, namshukuru kwa ukuu wake na upendo wake na kila jambo analolitenda na kuendelea kulitenda katika maisha yangu.

Wazazi wangu nao pia shukrani zangu ziwafikie popote walipo, lakini salamu na shukrani zangu ni kwenu mashabiki na wana familia wote wa Chelsea duniani kote na haswa kwa wale wanaotembelea ukurasa huu wa Darajani 1905.

Sasa leo, Darajani 1905 inafikisha familia yenye watoto (viewers) zaidi ya elfu kumi (10,000) kwa wiki moja ni hatua kubwa kwangu, lakini ni hatua kubwa zaidi kwa kila shabiki wa Chelsea maana mtandao huu unaotoa habari za Chelsea kwa lugha ya kiswahili umeleta mapinduzi.

Siliziki na wala sintobweteka kwa mafanikio haya ila hii ni kama kichocheo kwangu kunifanya nipige hatua zaidi ya kuwapa kile mnachostahili na mnachopaswa kukipata kama ukurasa bora wa Chelsea.

Nawashukuru wote, sina mengi ya kusema zaidi ya kusema Asanteni sana na msichoke kutembelea ukurasa huu ili kupata taarifa zote za Chelsea kutoka kwa shabiki nguli wa Chelsea
Facebook; Pacha wa Bakayoko
Facebook page; Chelseatz1905
Instagram; Pacha_wa_Bakayoko
Twitte

No comments:

Post a Comment