MRITHI WA MARCOS APATIKANA URENO - Darajani 1905

MRITHI WA MARCOS APATIKANA URENO

Share This

Kocha Antonio Conte amekuwa akitajwa kuumizwa kichwa kwa kumtafuta mlinzi wa upande wa kushoto atakayeweza kumpa changamoto Marcos Alonso anayecheza kwenye nafasi hiyo na kuonekana hana mpinzani.

Kennedy ambaye pia anacheza nafasi moja na Marcos Alonso anaonekana kushindwa kupambania nafasi hiyo huku pia akihusishwa kutakiwa na klabu kadhaa kwa mkopo.

Chelsea imekuwa ikitajwa kuwafukuzia nyota kadhaa kwenye nafasi hiyo huku mpango wake wa kumsajili mlinzi wa Juventus, Alex Sandro kuonekana kushindikana, sasa klabu hiyo imempata mrithi rasmi anayeweza kupambana na Marcos Alonso katika nafasi hiyo ya winga-mlinzi wa kushoto ambayo imekosa upinzani klabuni hapo.

Alex Telles wa klabu ya FC Porto ya nchini Ureno anatajwa kuwa kwenye rada za Chelsea ikimfukuzia kwa karibu ili kuweza kucheza kwenye nafasi hiyo.

Telles anatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa pasi za mwisho alishawai kutakiwa na Chelsea hapo kabla ila mpango huo uligoma na dili hilo likashindwa kutimia.

No comments:

Post a Comment