CHELSEA KUMNASA MWENGINE KUTOKA AS ROMA - Darajani 1905

CHELSEA KUMNASA MWENGINE KUTOKA AS ROMA

Share This
Klabu ya Chelsea inatajwa kumfukuzia nyota kuutoka klabu ya As Roma ya nchini Italia, Frorenzi. Ambaye amebakisha mkataba wa mwaka mmoja ili kumalizana na klabu yake hiyo. Frorenzi ambaye ni raia wa Italia anatajwa kutakiwa na Chelsea kwa karibu huku akitajwa kuondoka klabuni hapo katika dirisha kubwa la usajili.

Klabu kadhaa zinatajwa kuonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo mwenye uwezo pia wa kucheza kama mlinzi wa kati, ila Chelsea sasa ndio imeanza kutajwa kwa karibu kumnasa ikipambana na klabu za Juventus pamoja na AC Milan ambazo nazo zinamtaka nyota huyo mwenye miaka 26.

Kama Chelsea ikifanikiwa kumnasa nyota huyu, itakuwa imetimiza wachezaji watatu kuwanasa kutokea kwenye klabu hiyo toka Chelsea ilipokuwa chini ya kocha muitaliano, Antonio Conte. Wachezaji waliotoka kwenye klabu hiyo ambao tayari wameshatua Chelsea toka kuwepo kwa Conte ni pamoja na Antonio Rudiger pamoja na Emerson Palmieri.

No comments:

Post a Comment