UEFA YOUTH; CHELSEA KUCHEZA DHIDI YA MADRID - Darajani 1905

UEFA YOUTH; CHELSEA KUCHEZA DHIDI YA MADRID

Share This
Timu ya vijana chini ya miaka 19 ya Chelsea imeigaragaza klabu ya umri huo kutoka nchini Uholanzi, Feyenoord kwa magoli 5-2 na kufanikiwa kuvuka hatua ya 16 bora na kuingia katika robo fainali ambapo huko watasafiri mpaka kwenye jiji la Madrid na kucheza dhidi ya Real Madrid ya vijana wa umri huo katika michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa vijana, UEFA Youth Champions League.

Chelsea hiyo imepata ushindi wake huo muhimu huku Ethan Ampadu akionyesha kiwango cha hali ya juu akiwa pamoja na Callum Hudson-Odoi pamoja na Dejon Sterring.

Chelsea ya vijana imepata ushindi huo ikiwa nyumbani na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya robo fainali dhidi ya Real Madrid ambao wao wamefanikiwa kufudhu hatua hiyo mara baada ya kupata ushindi dhidi ya Bayern Munich ya vijana.

No comments:

Post a Comment