PLW; FRAN KIRBY AIPANDISHA CHELSEA KILELENI - Darajani 1905

PLW; FRAN KIRBY AIPANDISHA CHELSEA KILELENI

Share This
Klabu ya akina dada ya Chelsea maarufu kama Chelsea Ladies, leo imepata ushindi wake wa muhimu wa ligi kuu ya Uingereza kwa upande wa akina dada au wanawake ambapo imeibamiza klabu ya Yeovil magoli 0-2 ambapo Chelsea Ladies ilikuwa ugenini.

Shukrani kwa nyota wa mchezo huo, Fran Kirby (pichani) aliyefungua akaunti ya magoli kwa upande wa Chelsea Ladies mara baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwa sare ya bila kufungana. Fran Kirby alifunga goli hilo la muhimu kabla ya dakika chache tena Johannsen kufunga goli jengine la pili na kuifanya Chelsea Ladies kujihakikishia alama tatu.

Kutokana na matokeo hayo, Chelsea Ladies inafanikiwa kupanda katika msimamo wa ligi kuu kwa upande wa akina dada mara baada ya kufikisha alama 26 huku Man city Ladies wakiwa na alama 25.

No comments:

Post a Comment