HERI YA KUZALIWA IVANOVIC - Darajani 1905

HERI YA KUZALIWA IVANOVIC

Share This

Mwaka 2008, Chelsa ilikamilisha usajili wa mlinzi raia wa Serbia, Branislav Ivanovic kwa dau la paundi milioni 9. Leo nyota huyo anatimiza miaka 34 toka kuzaliwa kwake 22-Januari-1984.

Nyota huyo amefanikiwa kutwaa mataji kadhaa akiwa Chelsea ambapo atakumbukwa vyema kwa umahiri wake wa kucheza kama mlinzi wa kulia, lakini pia akitumika kama mlinzi wa kati akionekana imara kwa makocha wote waliowai kuifundisha Chelsea kwa kipindi ambacho nyota huyo alikuwa Chelsea kabla ya kuondoka klabuni hapo akijiunga na klabu ya nchini Urusi, Zenit St.Petersburg.

Nyota huyo ameiongoza Chelsea kushinda mataji kadhaa kama ligi kuu Uingereza, kombe la FA, kombe la ligi, Klabu bingwa Ulaya maarufu kama Uefa Champions League, lakini pia taji la Europa League mwaka 2013.

Mpaka anaondoka Chelsea aliweka rekodi kadhaa ikiwemo ya mmoja kati ya wachezaji watano kutoka nje ya Uingereza kucheza michezo nchini humo akiichezea Chelsea michezo 377 lakini pia akipitwa na John Terry tu katika rekodi ya ufungaji magoli mengi klabuni Chelsea, alifunga magoli 34. Lakini pia kwa uwezo wake mkubwa, ulimfanya kupewa unahodha kwenye timu yake ya taifa.

Hongera Ivanovic.

No comments:

Post a Comment