WILLIAN AGOMBANIA TUNZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA - Darajani 1905

WILLIAN AGOMBANIA TUNZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA

Share This
Nyota wa Chelsea, Willian da silva Borges amechaguliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombania uchezaji bora wa wiki mara baada ya kuiongoza vyema klabu yake katika usiku wa klabu bingwa Ulaya ambapo Chelsea ilicheza dhidi ya Barcelona, mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1 ambapo goli la Chelsea lilifungwa na mbrazili huyo aliyefunga mara baada ya kugongesha mwamba mara mbili.
Nyota huyo ameingia katika kinyang'anyiro hicho akishindania tunzo hiyo inayotolewa na chama cha soka barani Ulaya maarufu kama Uefa akishindana na nyota wengine watatu ambao ni mlinda mlango wa Manyumbu (Man utd), David de Gea, nyota wa Shakter Donetsk, Fred.
Ili kumpigia kura nyota huyo kushinda tunzo hiyo, bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment