WILLIAN AGOMBANIA TUNZO YA GOLI BORA - Darajani 1905

WILLIAN AGOMBANIA TUNZO YA GOLI BORA

Share This
Nyota wa Chelsea, Willian Borges ameingia pia kwenye tunzo ya kugombania goli la wiki katika michuano ya klabu bingwa Ulaya alilolifunga katika mchezo wa raundi ya 16 bora ambapo Chelsea ilimenyana dhidi ya Barcelona juzi jumanne ambapo mchezo huo uliisha kwa sare ya 1-1.
Nyota huyo ameingia kwenye kinyang'anyiro cha tunzo hiyo kugombania tunzo hiyo akiichezea Chelsea mchezo wa 50 kwa michezo yanayohusisha makombe na kufanikiwa kufunga goli hilo kabla mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Hii ni tunzo ya pili ambapo nyota huyo anashindania katika wiki hii ya klabu bingwa barani Ulaya ambapo tunzo ya nyengine anayoshindania ni tunzo ya mchezaji bora wa wiki.
Kwa kupiga kura ili kuchagua goli lake kuwa goli bora la wiki, bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment