COURTOIS KUONDOKA CHELSEA? - Darajani 1905

COURTOIS KUONDOKA CHELSEA?

Share This

Mlinda mlango wa Chelsea ambaye ni raia wa Ubelgiji, Thibaut Courtois amekuwa akitajwa kwa karibu kutakiwa na klabu ya Real Madrid huku akihusishwa kwa karibu kutua klabuni hapo kutokana na familia yake kuwa kwenye jiji la klabu hiyo, jiji la Madrid.

Familia ya nyota huyo ambao ni mke wake na watoto wake wawili wote wanaishi nchini Hispania kwenye jiji la Madrid ambapo Courtois aliwai kuishi jijini humo pindi alipotolewa kwa mkopo na kwenda kuichezea klabu ya Atletico Madrid na amekuwa akikiri kuwa moyo wake upo kwa familia yake inayoishi jijini humo.

Mchambuzi wa chombo cha habari cha michezo cha ESPN, Allejadro Moreno haamini kama usajili wa nyota huyo utakuja kukamilika kujiunga na klabu hiyo na badala yake labda Madrid watakuwa tayari kuendelea na mlinda mlango wao wa sasa, Keylor Navas na kama Thibaut ataondoka Chelsea basi labda ataenda kwenye klabu nyengine na sio kujiunga na wababe hao wa ligi kuu Hispania ambao pia ni mabingwa watetezi wa klabu bingwa Ulaya.

Thibaut Courtois aliwai kukaririwa akisema ingawa anacheza Chelsea ila moyo wake upo nchini Hispania kwenye jiji la Madrid ambapo kwa kauli hiyo ilitafsiriwa kuwa nyota huyo anataka kuungana na klabu hiyo ya Real Madrid lakini baadae alisikika akisema maneno yake hayakumaanisha kuwa hataki kuendelea kubaki Chelsea na ana furaha kuendelea kuwa mchezaji wa klabu hiyo ila maana ya maneno yake ni kwamba moyo wake upo jijini humo kutokana na kuwa familia yake inaishi kwenye jiji hilo.

No comments:

Post a Comment