CHELSEA YOUTH YAPANGIWA VIGOGO UEFA - Darajani 1905

CHELSEA YOUTH YAPANGIWA VIGOGO UEFA

Share This

Mara baada ya jana kupata ushindi mnono dhidi ya klabu ya vijana ya Feyenoord ya nchini Uholanzi katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa vijana, klabu ya Chelsea Youth ambayo ni maalumu kwa vijana wa akademi imepangiwa kucheza dhidi ya Real Madrid ya uwiano wao katika michuano hiyo kwa hatua ya robo fainali siku ya tarehe 14-Marchi.

Chelsea jana ilipata ushindi wa magoli 5-2 dhidi ya Feyenoord na kufanikiwa kuvuka vyema hatua hiyo, na sasa inajiandaa kucheza dhidi ya klabu ya vijana siku ambayo Chelsea FC itakuwa uwanjani kupambana dhidi ya Barcelona katika mchezo wa marudiano kwa hatua ya raundi ya 16 bora.

Chelsea Youth imekuwa na uwezo mkubwa ikivuka hatua ya makundi wakiwa wamepoteza mchezo mmoja tu ambao ulikuwa dhidi ya As Roma ya vijana, na baadae kurudisha kipigo hicho iliposafiri kwenda Roma ambapo huko walipata ushindi wa 1-2.

No comments:

Post a Comment