DE VRIJ AIKARIBISHA CHELSEA KWENYE MAZUNGUMZO - Darajani 1905

DE VRIJ AIKARIBISHA CHELSEA KWENYE MAZUNGUMZO

Share This

Nyota wa klabu ya Lazio inayoshiriki ligi kuu nchini Italia, Stefan De Vrij sasa ni kama amezikaribisha klabu zinazotajwa kumtaka ni kama ndio zianze mbio za kumuwania mlinzi huyo ambaye anataka kuondoka klabuni hapo ili kusaka mafanikio makubwa ambayo alikuwa akiyaota toka akiwa na ndoto za kuwa mchezaji. Hakuna mchezaji au mtu asiyependa kujiona akifanikiwa, na hicho ndicho kinachotokea kwa sasa kwa mlinzi huyo raia wa Uholanzi.

Nyota huyo alisema "Najua ni ngumu kuondoka kwa hali kama hii, haswa kwa mashabiki na klabu ya Lazio, lakini pale unapohitaji kupata mafanikio makubwa basi inakubidi ata uachane na kile kinachokufanya uwe bora" alisema mlinzi huyo ambaye ni raia wa Uholanzi na kwa sasa ana miaka 26 akiwa na uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa kati.

"Najua ni kwa kiasi gani nawaumiza mashabiki wa Lazio, lakini nina furaha ya kubaki hapa na kuendelea kupambana na kurudisha ile imani yao kwangu kwa kupigana na kutoa ubora wangu wote kwa ajili yao" alimaliza kwa kusema maneno hayo.

De Vrij ametajwa kwa karibu kutakiwa na Chelsea, lakini pia klabu nyengine vikitajwa kumuwania nyota huyo.

No comments:

Post a Comment