CHELSEA YATUA KWA NYOTA WA NEWCASTLE - Darajani 1905

CHELSEA YATUA KWA NYOTA WA NEWCASTLE

Share This

Klabu ya Chelsea inatajwa kumfukuzia nyota raia wa Uingereza anayeichezea klabu ya nchini humo, Newcastle united, Jamaal Lascelles mwenye miaka 24 kwa sasa.

Chelsea imekuwa ikivutiwa na nyota huyo anayecheza nafasi ya ulinzi wa kati kwa muda mrefu lakini sasa inatajwa kuanza mipango yake madhubuti ili kumnasa mlinzi huyo ambapo sababu kubwa inayotajwa kwa Chelsea kuingia sokoni ili kumsaka mlinzi wa kati ikitajwa kuwafukuzia nyota kama Samuel Umtiti na Stefan de Vrij ni kutokana na walinzi wake wa nafasi hiyo kuanza kutupwa mkono na umri wao ambapo Gary Cahill atatimiza miaka 33 mwezi Desemba wakati kwa David Luiz atatimiza miaka 31 ifikapo mwezi Aprili mwaka huu.

Lakini pia sababu inayotajwa kuivutia Chelsea kumchagua nyota huyu ni kutokana na uraia wake ambapo kwa Chelsea kumekuwa na upungufu wa wachezaji raia wa Uingereza klabuni hapo hali inayofanya kuendana tofauti na sheria ya ligi kuu nchini Uingereza na kwa sababu hiyo Chelsea inatajwa kuanza mipango ya kuwapa kipaumbele zaidi wachezaji wakiingereza na ndio sababu ya kuwasajili nyota kama Ross Barkley pamoja na Danny Drinkwater.

No comments:

Post a Comment