NYOTA WA CHELSEA AANZA KUWASHA MOTO - Darajani 1905

NYOTA WA CHELSEA AANZA KUWASHA MOTO

Share This
Nyota wa Chelsea, Kasey Palmer anayeichezea kwa mkopo klabu ya Derby County inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championship, jana aliifungia klabu hiyo goli lake la kwanza dhidi ya Leeds United, katika mchezo ulioisha kwa sare ya 2-2.

Nyota huyo mwenye miaka 21 aliyejiunga na klabu hiyo kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari akitokea klabu ya Huddersfield ambapo alikuwa huko kwa mkopo ameifungia klabu yake hiyo goli lake la kwanza na kutumia mtandao wa Twitter, kutuma ujumbe kuonyesha furaha yake juu ya goli lake hio.

"Nina furaha kwa kufunga goli langu la kwanza nikiwa Derby County dhidi ya Leeds United hapo jana. Sio matokeo tuliyoyategemea lakini naamini jumamosi tutapambana zaidi⚽🙏" alisema nyota huyo raia wa Uingereza.

Nyota huyo alijiunga na Chelsea katika timu ya vijana akitokea klabu ya Charlton mwaka 2013 na mpaka sasa hajafdanikiwa kuichezea Chelsea mchezo hata mmoja kwa ngazi ya timu ya kwanza na badala yake amekuwa akitolewa kwa mkopo na mpaka sasa ameshatolewa kwa mkopo kwenye klabu ambazo ni Huddersfield pamoja na Derby County aliyopo kwa sasa.

No comments:

Post a Comment