IVANOVIC AIBEBA TIMU YAKE KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA - Darajani 1905

IVANOVIC AIBEBA TIMU YAKE KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA

Share This
Jana ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mchezaji wa zamani wa Chelsea, Branislav Ivanovic ambaye aliichezea Chelsea kwa mafanikio makubwa akitwaa mataji yote katika ngazi ya vilabu ambapo alikuwa akitimiza miaka 34 toka kuzaliwa kwake. Nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya mlinzi wa kulia na wa kati, jana alikuwa uwanjani kupambana katika mchezo wa kombe la Europa ambapo ilikuwa ikicheza dhidi ya Celtic.

Katika mchezo huo, nyota huyo aliifungia klabu yake ya sasa ya Zenit St.Petersburg na kuiongoza vyema kupata ushindi wa magoli matatu huku Ivanovic akifunga goli moja. Ambalo lilikuwa ni goli la kwanza kwa klabu hiyo katika mchezo huo wa pili wa kugombania kufudhu kucheza raundi ya 16.

Nyota huyo alifunga goli hilo katika ushindi wa mabao 3-0 huku ikiwa ni siku pekee kwake akiwa anatimiza miaka 34 toka kuzaliwa kwake. Alijiunga na wababe hao wa nchini Urusi katika dirisha dogo la mwezi Januari mwaka uliopita mara baada ya kukosa nafasi ya uhakika katika kikosi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment