TOTTENHAM YAMWACHIA ALDERWIELD AJIUNGE NA CHELSEA - Darajani 1905

TOTTENHAM YAMWACHIA ALDERWIELD AJIUNGE NA CHELSEA

Share This
Chelsea imekuwa ikimfukuzia nyota wa klabu ya Tottenham, Toby Alderwield ambaye ni raia wa Ubelgiji ambaye kwa sasa ana miaka 28. Nyota huyo amekuwa akikosa nafasi ya uhakika katika kikosi cha kwanza mara baada ya klabu hiyo kumnasa nyota Davinson Sanchez kutoka klabu ya Ajax ambaye anaonekana kuwa na nafasi kubwa na kuaminiwa zaidi.

Nyota huyo amekuwa akihusishwa kutakiwa na Chelsea mara baada ya kukosa kwake nafasi klabuni Tottenham na sasa klabu hiyo iliyokuwa ikihofia kumuuza inaelezwa kuwa kwa sasa ipo tayari kumuachia kutokana na mahitaji ya nyota huyo kuonekana hayaendani na mahitaji ya klabu.

Nyota huyo analipwa kiasi cha paundi 150,000 kwa wiki kama kiasi cha mshahara wake na kama klabu inagoma kumlipa mshahara mnono kama huo mchezaji ambaye anatimiza miaka 29 ifikapo wiki ijayo. Huo ni umri mkubwa kwa kulipwa mshahara huo kama inavyoona klabu hiyo inayopatika kwenye jiji la London a hivyo kuonekana kuwa ipo tayari kumuuza ifikapo kipindi cha usajili cha dirisha kubwa mwisho wa msimu.

No comments:

Post a Comment