HAZARD AELEZA ALICHOMWAMBIA WILLIAN - Darajani 1905

HAZARD AELEZA ALICHOMWAMBIA WILLIAN

Share This
Mara baada ya mchezo wa ngwe ya kwanza ya klabu bingwa barani Ulaya kati ya Chelsea dhidi ya Barcelona ambao mchezo huo uliisha kwa sare ya mabao 1-1 ambapo Willian ndiye aliyechaguliwa kuwa nyota wa mchezo huku akiifungia goli moja klabu hiyo, nyota mwenzake klabuni hapo, Eden Hazard alieleza ni nini alichomwambia mchezaji huyo mara baada ya kipindi cha kwanza kuisha.

"Nilimwambia hatakiwi kugongesha mwamba, na badala yake apige ili afunge na kweli alifanya hivyo. Nilimwambia hivyo katika kipindi cha kwanza, na kipindi cha pili alifanya kama nilivyomwambia na akafunga. Ye ni mchezaji bora mwenye uwezo mkubwa, na ilo ametuonyesha, " alisema nyota huyo.

"Inatakiwa tuwe na ubora zaidi, tunatakiwa kucheza tuiwa na uhakika wa kutokuruhusu kufungwa na inatakiwa tufunge ili tuweze kusonga mbele. Bado tuna wiki tatu za kujiandaa kabla ya kucheza marudiano (dhidi ya Barcelona) na tutapambana kupigania nafasi yetu" alisema nyota huyo alipoulizwa juu ya nafasi ya Chelsea kufudhu kucheza hatua ya robo fainali ambapo mchezo wa marudiano utachezwa siku ya tareh 14-Marchi huko nchini Hispania.

No comments:

Post a Comment