RATIBA YA KOMBE LA FA KATI YA CHELSEA vs LEICESTER YAPANGWA - Darajani 1905

RATIBA YA KOMBE LA FA KATI YA CHELSEA vs LEICESTER YAPANGWA

Share This
Mara baada ya Chelsea kupata ushindi dhidi ya Hull city katika mchezo uliopita wa kombela FA kwa hatua ya raundi ya tano ambapo Chelsea ilipata ushindi wa magoli 4-0 na kufanikiwa kufudhu hatua hiyo, ikachezeshwa droo ili kupangwa hatua ya robo fainali ambapo Chelsea ilipangwa kucheza dhidi ya Leicester ciy katika hatua ya robo fainali.

Robo fainali hiyo haikutangazwa ni lini itatimua vumbi mpaka ilipofikia leo ilipotangazwa ratiba rasmi ya mashindano hayo huku Chelsea ikiapngwa kumenyana na wababe hao wa King Power siku ya tarehe 18-Marchi.

Tarehe hiyo itakuwa ni siku nne baada ya Chelsea kutoka nchini Hispania kucheza mchezo wake wa ngwe ya pili ya michuano ya klabu ya mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona ambapo mchezo huo utakuwa umechezwa siku ya tarehe 14-Marchi.

No comments:

Post a Comment