BATSHUAYI AWASHANGAA MASHABIKI BAADA YA KUITWA NYANI - Darajani 1905

BATSHUAYI AWASHANGAA MASHABIKI BAADA YA KUITWA NYANI

Share This
Nyota wa klabu ya Chelsea, Michy Batshuayi ambaye anaichezea klabu ya Borrusia Dortmund kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu huu amesema amejitokeza hadharani na kulalamika juu ya ubaguzi alioonyeshwa katika mchezo wa klabu yake hiyo aliyopo kwa mkopo ilipomenyana dhidi ya klabu ya nchini Italia, Atalanta katika mchezo wa Europa league ambapo mchezo huo uliisha kwa Dortmund kufudhu kwa magoli ya jumla3-4.

Michy Batshuayi alipohojiwa juu ya tuhuma izo alisema "Nilisikia kelele za mashabiki wakilia kama nyani. Nashangazwa kwa mambo kama haya kuendelea kutendeka haswa katika mwaka huu 2018"

"Mwaka 2018, na bado unaikia kelele za sauti ya nyani kwa mashabiki? kweli?" alihoji nyota huyo.

Mwezi uliopia klabu hiyo ilifungiwa mchezo mmoja mara baada ya kuonyesha ubaguzi kwa mchezaji Kalidou Koulibaly katika mchezo wa ligi kuu Italia. Lakini pia kumekuwa a mfululizo wa matukio ya ubaguzi wa rangi haswa katika ligi kuu nchini humo ambapo kwa nyakati tofauti tofauti kumewai kuripotiwa kuwepo matukio ayo, iliwai pia kumtokea mlinzi wa Chelsea, Antonio Rudiger alipokuwa nchini Italia alipokuwa akicheza kweye klabu ya As Roma, na hata usajili wake wa kutua Chelsea iliwai kudhaniwa umetokea kutokana na mchezaji huyo kuchoshwa na tabia hizo. Ila Rudiger alikana na kusema bado ana heshima kwa waitalia na sio kwamba ubaguzi wa rangi ndio umemfanya aondoke huku akisema sababu kubwa ya kutua Chelsea ni ili kusaka changamoto nyengine.

No comments:

Post a Comment