CONTE ASEMA CHRISTENSEN NDIYE NAHODHA - Darajani 1905

CONTE ASEMA CHRISTENSEN NDIYE NAHODHA

Share This
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte leo amefanya mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa jumapili ambapo Chelsea itakuwa ugenini kumenyana dhidi ya Manyumbu (Man utd) katika mchezo wa raundi ya 28 wa ligi kuu Uingereza, huku ukiwa ni mchezo wenye kuvuta hisia za wengi kutokana na vita ya maneno iliyokuwa ikendelea kati ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte dhidi ya Jose Mourinho, ambaye ni kocha wa zamani wa Chelsea wakati kwa sasa akiwa anaifundisha klabu hiyo ya Manyumbu.

Kuelekea kwenye mchezo huo kocha huyo Antonio Conte ameulizwa swali juu ya kosa alilolifanya mlinzi wa klabu hiyo, Andreas Christensen kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Barcelona ambapo nyota huyo alitoa pasi ambayo ilikuwa ikiambaambaa bila kujulikana ilikuwa ikienda kwa nani na kumfanya kiungo wa Barcelona, Andreas Iniesta kuuwai na kutoa pasi kwa Lionel Messi na kufunga goli la kusawazisha.

"Kwa upande wangu nishalisahau kosa hilo. kwake pia, ukiwa mchezaji kwenye maisha yako ya soka lazima ufanye makosa. Haijalishi iwe limetokea kwa namna gani, (Christensen) amekuwa na msimu mzuri na kuonyesha ukomavu wa hali ya juu. Namuamini na nadhani ataendelea kuwa mchezaji wa Chelsea ata kwa miaka kumi na anaweza kuwa nahodha wa Chelsea hapo baadae"

"Mchezo wa jumanne umetpa kujiamini sana na kutuonyesha kama tukiendelea kupamabana zaidi basi itakuwa ngumu kwa wapinzani kupambana dhidi yetu" alisema kocha Antonio Conte.

Lakini jana mlinzi huyo raia wa Denmark alipohojiwa juu ya kosa hilo alisema "Nimekuwa nikicheza kwa ubora mkubwa, lakini mwisho nimekuja kufanya kosa. Ingetakiwa ata nitolewe kwenye mchezo ule. Kama mlinzi, unaadhibiwa kutokana na makosa unayoyafanya. Nilitaka kucheza mpira ili tumiliki kama timu lakini mwisho nikafanya makosa. Najua nilifanya makosa, lakini hakuna jengine la kufanya zaidi ya kujirekebisha na kujifunza kutokana na kosa nililolifanya" aliseam nyota huyo.

No comments:

Post a Comment