VITA NYENGINE YA CONTE DHIDI YA ANCELLOTTI - Darajani 1905

VITA NYENGINE YA CONTE DHIDI YA ANCELLOTTI

Share This
Kuna mfululizo wa taarifa tofauti tofauti unaendelea huko mitandaoni kwa sasa, huku mfululizo mkubwa wa taarifa hizo ukimhusu kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambapo kikubwa kinachozungumzwa kwa sasa ni uwezekano wa kocha huyo kusalia klabuni Chelsea.

Magazeti ya Guardian na Telegraph ya nchini Uingereza yanaamini kocha huyo ataendelea kuwepo klabuni Chelsea, lakini kuna taarifa tena zimetoka kupinga habari hizo za magazeti hayo zikieleza kuwa kocha huyo anatazamiwa kuungana na timu ya taifa ya Italia ambako huko ndiko anapotokea kocha huyo.

Makamu kamishna wa chama cha soka cha Italia (FIGC), Costacurta alisema "Nitasafiri mpaka London kwenda kuongea na Conte juu ya uwezekano wake wa kurudi kuifundisha Italia ambapo pia hukohuko nitakutana na Carlo Ancellotti (alishawai kuifundisha Chelsea), kwa maana hiyo wote nitaongea nao"

"Antonio (Conte) aliiongoza vyema Italia katika michuano ya Euro na bado anaendelea kufanya kazi nzuri. Kiufupi, anaweza kuwa kocha wa Italia kwa mara nyengine. Hatutakiwi kukaa muda mrefu kumsubiri kocha atakayevaa viatu vya Ventura, lakini inabidi tufanye maamuzi sahihi katika hili"

"leno letu ni kuirudisha Italia inayostahili kuwepo kutokana na historia na tamaduni zake" alisema kamishna huyo.

Taarifa hii inakuja mara baada ya kutoka taarifa hapo mwanzo ambayo hata humu nimekuletea ikimhusu rais wa chama hicho akimtaja Antonio Conte kama mmoja ya makocha wanaotazamiwa kuifundisha timu ya taifa ya Italia, kuisoma taarifa hiyo bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment