CONTE ATAMANI KURUDI ITALIA - Darajani 1905

CONTE ATAMANI KURUDI ITALIA

Share This
Mara baada ya koocha Antonio Conte kuhusishwa kwa karibu kuondoka klabuni Chelsea, kumetoka tena taarifa mpya inayopingana na taarifa iliyotolewa na magazeti ya Guardian na Telegraph ya nchini Uingereza ambayo yenyewe yalitoa taarifa kwa kocha Antonio Conte kuendelea kusalia klabuni Chelsea (Kusoma taarifa hii kwa urefu bonyeza hapa) lakini taarifa tena mpya imeripotiwa juu ya hatma ya kocha huyo klabuni Chelsea akihusishwa kutaka kujiunga tena na timu ya taifa ya Italia.

Taarifa hiyo imetolewa na rais mpya wa chama cha soka cha nchini Italia (FIGC), anayeitwa Roberto Fabricini akisema kocha Antonio Conte anatamani kurudi kwenye timu ya taifa ya nchi hiyo "Majina yanayoweza kuchukua majukumu hayo huenda akawa Roberto Mancini ambaye alikuwa Roma ingawa hatujafanya mawasiliano naye, Conte ni kama anatamani kurudi tena kuifundisha timu ya taifa, Carlo Ancellotti ni kama alifungua milango ila baadae akaifunga na hata Claudio Ranieri inaonekana hapatikani" alisema rais huyo alipoulizwa ni nani atachukua nafasi ya ukocha katika timu ya taifa ya nchini humo. Ambapo timu hiyo kwa sasa haina kocha kutokana na kocha aliyekuwepo Gian Piero Ventura kuachana na timu hiyo mara baada ya kushindwa kuisaidia kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka huu uko nchini Urusi.

Kocha Antonio Conte aliwai kuifundisha Italia toka mwaka 2014 mpaka mwaka 2016 ambapo kuanzia hapo akatangazwa rasmi kuwa kocha wa Chelsea.

No comments:

Post a Comment