CONTE KUONDOKA CHELSEA? - Darajani 1905

CONTE KUONDOKA CHELSEA?

Share This
Kabla na hata baada ya mfululizo wa matokeo mabaya kwa Chelsea kumekuwa na taarifa na fununu zikiendelea pale klabuni Chelsea zikimhusisha kocha wa klabu hiyo Antonio Conte kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu lakini kuna taarifa mpya imetolewa na magazeti ya nchini Uingereza juu ya hatma ya kocha huyo raia wa Italia.
Magazeti ya Guardian na Telegraph yameripoti kuwa hakuna uhusiano wa fununu hizo juu ya kocha huyo na wanatazamia kocha huyo kuendelea kubaki klabuni hapo.
Magazeti hayo yanaamini kocha Antonio Conte bado ana nguvu na ushawishi mkubwa klabuni hapo haswa kwa mashabiki wakionekana kuvutiwa nae na kuliimba jina lake hata baada ya mchezo uliopita dhidi ya Afc Bournemouth ambapo Chelsea ilipoteza ikiwa nyumbani kwa magoli 3-0. Hii ni tofauti na makocha wengine waliowai kupita Chelsea na kupata matokeo yasiyolizisha na bado wakapata ushirikiano kutoka kwa mashabiki kama inavyotokea kwa Antonio Conte.
Kuna makocha wanatajwa kwa karibu kuchukua nafasi ya kocha Antonio Conte klabuni Chelsea ambapo inatajwa aliyekuwa kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique akiwa mmoja wapo ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi ya Conte lakini magazeti hayo hayaamini kama kocha huyo atatua klabuni hapo. Wengine wanaohusishwa ni pamoja na Carlo Ancellotti ambaye kwa sasa hana timu, Massimiliano Allegri ambaye ni kocha wa Juventus na kocha wa Napoli, Maurizio Sarri.

No comments:

Post a Comment