DZEKO ATOA NENO KUHUSISHWA NA CHELSEA - Darajani 1905

DZEKO ATOA NENO KUHUSISHWA NA CHELSEA

Share This
Chelsea imefanikiwa kumnasa mshambuliaji wa kati, Olivier Giroud ambapo iliaminika tatizo au nafasi ya Chelsea ambayo inatatizo kwa sasa ni katika nafasi hiyo ya ushambuliaji, na sasa amepatikana nyota huyo raia wa Ufaransa kabla kufungwa kwa dirisha dogo la usajili lililofungwa hapo juzi.
Lakini kabla ya kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 31 kwa sasa, alishawai kutakiwa mshambuliaji raia wa Bosnia, Edin Dzeko ambaye anaichezea klabu ya As Roma ya nchini Italia, lakini mpango huo ukashindikana siku kadhaa kabla ya dirisha kufungwa na ndipo Chelsea ikamnasa Olivier Giroud kutoka Arsenyani (Arsenal).
Mshambuliaji huyo ambaye mpaka sasa ameifungia klabu yake ya As Roma magoli 13 huku akiifunga Chelsea magoli mawili katika mchezo wa makundi wa klabu bingwa Ulaya alihojiwa na chombo kimoja cha habari cha nchini kwao Bosnia aliulizwa juu ya kutakiwa kwake na Chelsea.
"Ilikuwa ni jambo zuri kwangu kutakiwa na Chelsea maana naiheshimu sana, ni kweli kulikuwa na mazungumzo kati ya pande mbili ili nijiunge nayo, ila kuna baadhi ya taarifa zilikuwa zinatolewa kinyume katika usajili huu" alisema nyota huyo ambaye alishawai kucheza Uingereza akiichezea klabu ya Mama site (Manchester city).
Alipoulizwa juu ya mahusiano yake na klabu yake ya As Roma yapo vipi, alisema "Roma kwangu imekuwa kama nyumbani, na nafurahi kuwa hapa maana pamekuwa ni sehemu muhimu zaidi kwenye maisha yangu"
Je unadhani  ni lipi chaguo sahihi Olivier Giroud au Edin Dzeko?

No comments:

Post a Comment