Michezo ya kirafiki kwa timu za taifa kabla ya michuano ya kombe la dunia kuanza bado inaendelea huku baadhi ya nyota wa Chelsea wakiungana na timu zao za taifa ili kucheza michezo ambayo baadhi ya timu za taifa zinazoshiriki michuano hiyo ya kombe la dunia ikiitumia michezo hiyo kama michezo ya kujiandaa na kuvitengeneza vikosi vyao kabla ya kuanza kwa michuano hiyo iliyobakiza siku saba kabla ya kuanza.
Usiku wa jana kulichezeka michezo miwili iliyowahusisha nyota wa Chelsea na kama ilivyoada hapa nakuletea muhtasari wa nini kilitokea katika michezo hiyo kuhusu nyota wa Chelsea.
Nigeria 0-1 Jamhuri ya Czech
Nyota wa Chelsea aliyeitumika kwa mkopo kwenye klabu ya Fulham kwa misimu miwili, Tomas Kalas alihitaji dakika 25 tu kuweza kuifanya timu yake hiyo ya taifa kuondoka na ushindi huo mwembamba wa goli 0-1 na kuisababisha Nigeria kupoteza mchezo wake wa pili mfululizo mara baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Uingereza. Kwa upande wa Nigeria, Victor Moses alikuwemo kwenye mchezo huo sambamba na kiungo wa zamani wa Chelsea, John Obi Mikel wakati nyota wengine kama Keneth Omeruo na Ola Aina wakikosa nafasi ya kucheza.
Ubelgiji 3-0 Misri
Eden Hazard ameiongoza vyema timu yake ya taifa ya Ubelgiji kupata ushindi mnono dhidi ya timu hiyo ya Mafarao wa Afrika, Misri.
Goli lake moja na akitengeneza goli jengine kwa kutoa pasi ya goli linamfanya nyota huyo kuipa timu yake ushindi mnono wa magoli 3-0 huku nyota wengine wa Chelsea, Thibaut Courtois pamoja na Michy Batshuayi walipata nafasi ya kucheza ambapo Batshuayi aliingia kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 46'
Mchezo wa leo wa kirafiki utakaomhusisha nyota wa Chelsea ni Uingereza watakaocheza dhidi ya Costa Rica ambapo Gary Cahill na Ruben Loftus-Cheek wataiongoza timu yao hiyo ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment